Shule ya awali na msingi Miyuji, Dodoma
0765 884 788 brmartinschool2016@gmail.com
SW EN

ELIMU · UDUGU · HUDUMA

Brother Martin Pre & Primary School

P.O. Box 1522 – Dodoma, Tanzania

“Feed the mind, free the child.”

TAARIFA YA SHULE Karibu Brother Martin Pre & Primary School Elimu ya kutwa na bweni inayojenga maarifa, udugu na uwajibikaji.

NDUGU WADOGO WAKAPUCHINI · TANZANIA

Karibu katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Miito

Safari ya wito huanza kwa sala, kutafakari na kuwa tayari kuhudumia wengine.

“Sema, Bwana, mtumishi wako anasikia.”

Ndugu Wakapuchini katika maisha ya sala na huduma
Fr. Phestus Manda, OFM Cap.Mkurugenzi wa Miito

UJUMBE WA OFISI

Wito ni safari ya kutafakari na huduma

Karibu katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Miito ya Ndugu Wadogo Wakapuchini. Wito wa maisha ya kikapuchini hukua katika sala, maisha ya kindugu, huduma kwa watu na utayari wa kuitikia Injili. Ofisi hii ipo kuwasaidia vijana na familia kupata mwongozo sahihi, kuuliza maswali, kuandika barua ya maombi na kufahamu hatua zinazofuata. Kutuma barua hakumaanishi kuchaguliwa moja kwa moja; kila ombi hupitiwa kwa umakini na mwombaji anaweza kualikwa kwenye semina ya kufahamiana Dodoma–Miyuji. Karibu uanze safari hii kwa sala, ukweli na moyo wa kujifunza.

Soma ujumbe wote ↗

NJIA ZA KUFUATA

Anza na hatua inayolingana na elimu yako

✦

Nimemaliza / ninamalizia Darasa la Saba — kuomba Form One (Franciscan Seminary, Maua)

Barua inaeleza nia, majina, umri, parokia na shule ya msingi.

✦

Kidato cha Nne — kuomba kuzingatiwa kwa Form Five (Franciscan Seminary, Maua)

Matokeo ya Kidato cha Nne na mwelekeo wa masomo hupitiwa na uongozi husika.

✦

Nimemaliza Kidato cha Sita

Ambatisha taarifa za elimu na ueleze kwa nini unataka kuendelea na safari ya malezi.

✦

Nina Diploma

Ambatisha taarifa za elimu na ueleze kwa nini unataka kuendelea na safari ya malezi.

✦

Chuo kikuu / chuo cha kati (GPA)

Ambatisha taarifa za elimu na ueleze kwa nini unataka kuendelea na safari ya malezi.

✦

Njia nyingine ya elimu

Ambatisha taarifa za elimu na ueleze kwa nini unataka kuendelea na safari ya malezi.

Mahitaji mahususi na nafasi hutegemea taasisi husika. Kutuma barua si ahadi ya kuchaguliwa.

Soma mwongozo wote ↗

ELIMU NA MALEZI

Shule mbili za malezi

Franciscan Seminary, Maua
Sekondari — Kidato I–VI

Franciscan Seminary, Maua

Maua, Moshi Vijijini, Kilimanjaro

Seminari ya malezi ya sekondari inayoendeshwa na Wakapuchini wa Tanzania, ikiwa na malezi ya kiakili, kiroho na kijamii. Kwa masharti na tarehe za sasa, tumia tovuti rasmi ya shule.

Tovuti/taarifa rasmi ↗
Capuchin Boys Secondary School
Sekondari

Capuchin Boys Secondary School

Pangani, Tanga

Shule ya sekondari ya wavulana inayoendeleza elimu katika utamaduni wa Kifransisko.

Tovuti/taarifa rasmi ↗
Taarifa za shule ↗

HATUA INAYOFUATA

Una swali au una barua ya kuwasilisha?

Wasiliana na ofisi au tuma barua yako, kisha hifadhi tracking code ili kufuatilia hatua zinazofuata.